ARSENAL FANS TZ

HABARI WAUNGWANA:

Tumeamua kuandika Description ya hii group kwa Lugha ya kiswahili ili kila mmoja aelewe nini kinahitajika na nini hakihitajiki kwenye Hii Group Page:

1. Member yeyote wa hii group ana haki ya kutoa mawazo yake kutoa wazo lake lolote ambalo anahisi kwamba ni la kujenga au la kukosoa mwenendo wa timu yetu.... sote tunaelewa kwamba binadamu wote hakuna aliye mkamilifu kwa maana hii hatuwezi kukwepa kuyaongelea mabaya yaliyopo katika hii timu yetu na hii haimuondolei mtu haki ya kuwa arsenal supporter.

2. Si vema sisi kama wana Jumuiya kutukanana na kutoleana maneno ya kejeli ambayo tunahisi kwamba yataleta migongano kati yetu... si vema kumtolea maneno makali mwanachama mwenzako wa group eti tu kwa kuwa ametoa mawazo yake.. Binadamu hatufanani na kila mtu ana upeo wake wa kufikiri naomba tuzingatie hili.

3. Humu hamna mipaka ya lugha ... Kingereza na kiswahili ndio lugha ambazo tunazipa kipaumbele hasa kutokana na kwamba zina wazungumzaji wengi (haulazimishwi kutumia kiswahili pekee ama kingereza pekee)

4. Jamani tujifunze kuweka page yetu iwe safi muda wote... Post ambazo tunahisi hazihusiani na group hii si vema tukawa tunaziposti ati tu kwa matakwa yetu sisi... namna hiii tutakuja kujenga utengano kati yetu...Group inasema Arsenal fans tz ina maana post ambazo ni related na arsenal ndio zinahitajika.. members wanaweza kuposti habari nyingine ambazo tunahisi kwamba ni za ulazima na kwa wakati huo zinaonekana zimeshika kasi katika vyombo vya habari kama World Cup, Euro, Afcon n.k.

5. Mimi sioni kama kuna ulazima wa member kuposti kitu kinachomuhusu member mwenzake, nafikiri hii tutakuwa tunakwenda kinyume na utaratibu na tunavunja sheria no 2 ya group hii. Sisi kama fans wa arsenal ni kama familia moja kwanini tusiishi kwa amani?? hata kama hatutaelewana ni kwa maslahi ya club tu hii inaeleweka (anti-wenger & pro-wenger) hawa wote wanatakiwa kwa group.

HAPO TUMEMALIZA
Admins board.